JIFUNZE KILIMO CHA MBAAZI (PIGEON PEAS)
Utangulizi Mbaazi ni zao la chakula ambalo pia linaweza kulimwa kama zao la biashara kutokana na kuwa na soko zuri la Mbaazi.Mbaazi ina kiasi kikubwa cha protini.Mbaazi inaweza kutoa mavuno ya tani 3.5 hadi 4 kwa hekta HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI Mbaazi zinafaa kulimwa katika maeneo ya ukanda wa chini kutoka usawa wa bahari na pia hata sehemu za nyanda za juu nazo zinafaa kulimwa zao hili. Ni zao linalostahimili ukame na hili linalifanya kulimwa hata katika maeneo yanayopata mvua za wastani na yale yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.Mbaazi hukua vizuri katika maeneo yenye wastani wa mua wa mm 400-1000 kwa mwaka,katika maeneo yenye mvua zaidi ya mm 1000 kwa waka hustawi ila ni rahisi kupta ugonjwa wa mnyauko.Mbaazi hustawi vizuri katika hali ya joto ya nyuzi 18-30 C. Pia kama hali ya udongo na unyevu ni nzuri zinaweza kukua vizuri katika hata katika 35 C. UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA MBAAZI Mbaazi zinastawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao...