Posts

Showing posts from July, 2018

Kilimo Bora cha Nyanya, Lima Kitaalamu na Kibiashara

Image
Utangulizi: Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu. Mazingira  Hali ya Hewa: Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.) Udongo: Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 – 7.0. Aina za Nyanya Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili: 1. OPV (Open Pollinated Variety) – Aina za kawaida. Mfano Tanya, Mwanga, Onyx n.k 2. Hybrid – Chotara: Hizi ...

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Ya Kufuga Kuku Yenye Mafanikio

Image
Tanzania ni nchi yenye walaji wa nyama wengi na kuku huliwa kwa kiasi kikubwa sana. Hata kama bei zinapanda, ulaji unaendelea kukua. Matokeo yake ni kwamba kufuga kuku inaweza ikawa biashara yenye faida kubwa kwako kwa kuwa yanahitajika kwa wingi. Kwa nini ufugaji wa kuku inafaida sana? Kuku haina madhara mengi ya kiafya kama nyama ya ng’ombe na watu wengi wanazidi kutambua hilo Kuku wanakua kwa kasi kwa hiyo unaweza ukapata mapato makubwa kwa kipindi kifupi. Kuku hailiwi nyumbani tu lakini pia kwenye migahawa, baa, hoteli na huduma zingine mbalimbali za chakula. Kwa hiyo kama una nia ya kuanzisha biashara ya kufuga kuku, inabidi uchukue hatua zifuatayo: 1. Chagua aina ya kuku: Kuna aina nyingi ya kuku, zikiwemo: Kuku wa kienyeji Bata Bata Mzinga Kanga Bata Bukini Tombo Kwa sasa, tutaweka maelezo yetu kwa Kuku wa Kienyeji. 2. Amua unataka kufuga kuku kwa malengo gani ya kibiashara Unaweza kufuka kuku kwa ajili ya biashara nyingi, zikiwemo: Kuku wa kuuza ...

MUONGOZO WA JINSI YA KULIMA PAPAI

Image
UTANGULIZI Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi. Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili. KUHUSU MPAPAI Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu i) Mpapai wenye maua kiume tu ii) Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya) Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe. Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika m...

Kilimo Cha Zao La Choroko

Image
Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium.Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari. Udongo na hali ya hewa  Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji. Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame. Aina za Choroko Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani. A) Choroko zinazotambaa , hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali. B) Choroko zinazosimama, hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusimama kwenda juu. Kipindi kizuri cha upandaji wa choroko Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga. Nafasi cha upandaji wa choroko na kiasi cha mbegu Choroko huit...

KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO

Image
UTANGULIZI Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. viazi mviringo vina virutubisho  vingi mfano vitamin, protin,madini na maji            SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku  mfano wa viazi mviringo AINA BORA YA VIAZI MVIRINGO Kuna aina nyingi sana ya viazi mviringo lakini hapa nitataja aina ambazo nazifahamu na ni bora kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole baraka sasamua tana subira(EAI 2329) Bulongwa kikondo(CIP 720050)      ...

👉 Ufugaji wa nguruwe na faida zake👇✔

Utangulizi Nguruwe ni mnyama amabaye hutumika kama chakula / mbonga na pia ni zao la biashara kwa mfugaji, mjasirimali na mfanyabiashara. NGURUWE HUTEGEMEA SANA MAMBO YAFATAYO 1 . Bada imara na rafiki kwake 2. Usafi ni muhimu sana katika bada la Nguruwe 3 Mchaganyo bora wa chakula 4. Tiba bora na kinga 5. Maji na Lishe ( access ya vyakula Muhimu kwake ) CHANGAMOTO KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE KUNACHAGAMOTO ZAKE LAKINI ZAWEZA KUTATULIWA KWA KUFATA MAMBO KADHAA. Katika ufugaji wa nguruwe kunachagamoto ya vifo vya nguruwe wachanga ambao hupunguza faida ya biashara ya nguruwe kwa kupunguza idadi ya nguruwe wazima wa kuuzwa lakini utunzaji mzuri wa nguruwe wachanga huepusha vifo vinavyotokana na shida kama: Matatizo ya kupumua Ni kifo kinachosababishwa na mama anapomlalia nguruwe mchanga.chagamoto hii inaweza kutatuliwa kwa kuwatega au kuwa na mabanda makubwa ya kulelea watoto. Baridi Nguruwe wachanga huathiriwa na baridi haswa katika majuma mawili au matatu ya mwanzo. Hii...

KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO

Image
 UTANGULIZI Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. viazi mviringo vina virutubisho  vingi mfano vitamin, protin,madini na maji             SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku        mfano wa viazi mviringo AINA BORA YA VIAZI MVIRINGO Kuna aina nyingi sana ya viazi mviringo lakini hapa nitataja aina ambazo nazifahamu na ni bora kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole baraka  ...

FAHAMU NAMNA NZURI YA KUVUNA MAJI YA MVUA KWA AJILI YA KILIMO NA MIFUGO

Image
Katika maeneo mengi ya Afrika mashariki hususani Tanzania tuna kiasi  kikubwa sana cha maji kwenye mito, chemichemi, maziwa na maji ya ardhini(undergroundwater) ambapo asilimia 70% hutumika kwenye kilimo kwa kuzalisha mazao mbalimbali Lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi mvua iliyokuwa ikitegemewa sana na wakulima kama chanzo cha maji kwa mimea imekuwa sio ya kuaminika tena kwani hainyeshi tena kwa wakati, hunyesha kwa kiasi kidogo sana(450mm-600mm), maeneo mengine hunyesha kwa kiasi kikubwa sana mpaka kusababisha mafuriko ambayo huharibu vibaya mazao ya wakulima mashambani, pia baadhi ya vyanzo vya maji vimekauka na hivyo kusababisha uhaba mkubwa sana wa maji sio tuu kwenye kilimo bali hata kwenye upatinaji wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani KWA NINI TUVUNE MAJI YA MVUA Kama nilipoeleza hapo awali kuwa kuna baadhi ya maeneo mvua hunyesha kwa kiasi kidogo sana na hivyo hazitoshelezi kumalizia msimu mzima ili mazao yaliyo shambani yaweze ku...