KILIMO CHA PILIPILI MANGA


Pilipili manga punde tu baada ya kuvunwa

Pilipili manga punde tu baada ya kuvunwa
Pilipili manga punde tu baada ya kuvunwa

Pilipili manga iliyoanikwa juani
Pilipili manga iliyoanikwa juani
Pilipili manga iliyoanikwa juani
 Maruk Vanilla, kampuni ya wakulima wa Kagera wenye malengo yanayoshabihiana katika kukuza mazao mbadala ya kibiashara mwaka huu imeshiriki msimu wa mavuno na ununuzi wa pilipili manga Mkoani Tanga.

Maruk Vanilla ambayo kwa Kagera inajihusisha zaidi na ukulima pamoja na ununuzi wa mapodo ya vanilla imedhamilia kwa dhati kuhakikisha Kagera pia inakuwa mzalishaji mkubwa wa pilipili manga.

Akitetea dhamira hii Mkurugenzi Mtendaji wa Maruk Vanilla Bwana Murshid Hassan alisema, “hali ya hewa
 ya Tanga inafanana na ya Kagera. Vilevile mazao yanayoshamili kwenye ardhi ya Kagera yanastawi vema pia Tanga. Hivyo tuna imani kubwa kwamba pilipilimanga itafanya vema kabisa Kagera.”

Bw. Murshid aliongeza pia kwamba zaidi ya miche 400 iliyosambazwa na Kampuni yao kwa majaribio kwa wakulima wa Bukoba, mingi imeendelea vema na kutia moyo.

Pilipili manga inayosubiri kufungwa tayari kwa kusafirishwa

Pilipili manga inayosubiri kufungwa tayari kwa kusafirishwa

Kuhusu kilimo na biashara ya pilipili manga
Pilipili manga ni zao linalochukua miaka miwili hadi mitatu kuanza kutoa matunda.
Kadiri mti unavyozidi kukua ndivyo na uwezo wake wa kuzalisha unavyoongezeka.
Tofauti na mazao mengine ya biashara, pilipili manga ni zao lisilohitaji nguvu sana kulistawisha wala muda mwingi wa kulishughulikia.
Soko lake ni kubwa sana ndani na nje ya nchi.
Pilipili manga hutumika kama kiungo cha vyakula. Mathalani kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu, Waislamu wengi hutumia kiungo hiki katika uji.
Kama ilivyo kwa mazao mengine, uzalishaji wetu wa ndani wa pilipili manga hautoshelezi mahitaji. Hivyo Tanzania huagiza tani za zao hili kutoka India na Pakistan.
Maruk Vanilla wanatoa wito kwa wakulima pamoja na wadau wote wa maendeleo wenye nia ya kutaka kujiunga na kuvumisha ukulima wa pilipili manga mkoani Kagera kuunganisha nguvu. Kwa sasa Maruk Vanilla wanaendelea na jitihada za kuandaa vitalu vikubwa vya miche ya pilipili manga.

Uvunaji  wa pilipili manga ukiendelea...

Uvunaji wa pilipili manga ukiendelea...

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU NAMNA NZURI YA KUVUNA MAJI YA MVUA KWA AJILI YA KILIMO NA MIFUGO

UFUGAJI BORA WA SAMAKI

KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI