Posts

BAADHI YA MISEMO NA METHALI TOKA TANZANIA

Image
1. Acha kukuna makovu ya mende (Kichaga) Maana yake ni kwamba uache kukumbuka taabu ya wakati uliopita. Methali hii itafahamika vizuri kama tukielewa kwamba hapo zamani katika jamii zetu, mende walikuwa wanaonekana kwa wingi katika nyumba. Nao mende ni hodari wa kuuma watu wakati wa usiku wakiwa wamelala. Na pale walipouma hubaki kovu ambalo hukuna. Lakini pia ambaye ameshaumwa na mende hao itakuwa ni kazi bure kama atakalia kuyakuna makovu hayo. Methali hii hutumika kwa kuwaonya watu wasikalie kufikiria makosa au taabu za wakati uliopita. 2. Afadhali kuchakaza nguo kuliko akili (Kipare) Maana yake ni kuwa hakuna kitu bora kama akili (hekima). Mtu ambaye hana hekima ya uchi kuliko uchi wa aina yoyote ile. Kuwa uchi kinguo, mtu anaweza kununua zingine. Lakini mtu anapokuwa uchi kiakili, hakuna maarifa. Methali hii hutumika kwa kumhurumia mtu ambaye ameharibikiwa na akili na anafanya majambo isivyotakiwa katika jamii. 3. Amekufa hata Mwakafwile aliacha mwana alipokufa (Kinyaky...

FURSA KWENYE KILIMO CHA MUHOGO

Image
Habari za leo mjasiriamali wa Kilimo. Leo napenda kukuletea somo kuhusu kilimo cha  Muhogo . Kama kawaida kazi yangu kubwa ni kuhakikisha unafanikiwa kwenye eneo la kilimo, kwa kukuletea elimu sahihi na fursa mbalimbali zinazohisiana na Kilimo. Wiki iliyopita tuliangazia kwa kifupi fursa ya kilimo cha Papai. Leo nitapenda tuangazie fursa ya kilimo cha Mihogo. Je wajua China na Tanzania zimesaini Mkataba wa Soko la Mihogo? Kama hufamu basi nikuelezee kwa ufupi. Ni hivi, Nchi ya China ni moja ya nchi zinazotumia sana zao la  muhogo.  China imeingia mkataba na Serikali ya Tanzania wa soko la mihogo, ambapo Tanzania itapaswa kuuza China mhogo Tani laki moja (100,000) kwa mwaka. Hata hivyo toka mkataba huo usainiwe hadi leo mwaka mmoja tayari umepita. Ila kwa mwaka wa kwanza, Tanzania tulifanikiwa kuuza tani 10,000 pekee (sawa na asilimi 10% tu ya kiasi kinachohitajika). Hivi karibuni nilimsikia Balazi wa China nchini Tanzania, Wang Ke akisema, licha ya kuingia makubalian...

JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU SEHEMU YA KWANZA(1

Image
Karibu mpenzi msomaji wa  KILIMO TANZANIA  , leo hii napenda kuwaletea soma la jinsi ya kulea vifaranga vya kuku, hivyo tusiache kua nasi ili kujifunza mengi zaidi. Na tutaanza na jinsi ya kujenga nyumba ya vifaranga, hivyo ukitaka kujenga nyumba ya vifaranga nilazima uzingatie yafuatayo. Nyumba ya vifaranga nilazima ijengwe karibu na nyumba ya muangalizi hii ni kwaajiri ya kuweza kuwa karibu kwa uangalizi zaidi. Nyumba ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa hii nikwaajili ya kupunguza maambukizi ya magonjwa. Nyumba ya vifaranga isiruhusu unyevu, baridi na wanyama au wadudu kuingia ndani, lakini ni lazima iwe na mwanga wakutosha Pia nyumba ya vifaranga inatakiwa kua na uwazi wa kutosha kuwezesha vifaranga kutobanana na waweze kutembea kwa uhuru. pia ijengwe eneo ambalo haliruhusu upepo kutoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa kuingia hii itapunguza maambukizi ya magonjwa. NJIA RAHISI UNAYOWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA   UKUBWA WA N...

Kilimo Bora cha Nyanya, Lima Kitaalamu na Kibiashara

Image
Utangulizi: Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu. Mazingira  Hali ya Hewa: Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.) Udongo: Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 – 7.0. Aina za Nyanya Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili: 1. OPV (Open Pollinated Variety) – Aina za kawaida. Mfano Tanya, Mwanga, Onyx n.k 2. Hybrid – Chotara: Hizi ...

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Ya Kufuga Kuku Yenye Mafanikio

Image
Tanzania ni nchi yenye walaji wa nyama wengi na kuku huliwa kwa kiasi kikubwa sana. Hata kama bei zinapanda, ulaji unaendelea kukua. Matokeo yake ni kwamba kufuga kuku inaweza ikawa biashara yenye faida kubwa kwako kwa kuwa yanahitajika kwa wingi. Kwa nini ufugaji wa kuku inafaida sana? Kuku haina madhara mengi ya kiafya kama nyama ya ng’ombe na watu wengi wanazidi kutambua hilo Kuku wanakua kwa kasi kwa hiyo unaweza ukapata mapato makubwa kwa kipindi kifupi. Kuku hailiwi nyumbani tu lakini pia kwenye migahawa, baa, hoteli na huduma zingine mbalimbali za chakula. Kwa hiyo kama una nia ya kuanzisha biashara ya kufuga kuku, inabidi uchukue hatua zifuatayo: 1. Chagua aina ya kuku: Kuna aina nyingi ya kuku, zikiwemo: Kuku wa kienyeji Bata Bata Mzinga Kanga Bata Bukini Tombo Kwa sasa, tutaweka maelezo yetu kwa Kuku wa Kienyeji. 2. Amua unataka kufuga kuku kwa malengo gani ya kibiashara Unaweza kufuka kuku kwa ajili ya biashara nyingi, zikiwemo: Kuku wa kuuza ...

MUONGOZO WA JINSI YA KULIMA PAPAI

Image
UTANGULIZI Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi. Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili. KUHUSU MPAPAI Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu i) Mpapai wenye maua kiume tu ii) Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya) Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe. Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika m...

Kilimo Cha Zao La Choroko

Image
Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium.Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari. Udongo na hali ya hewa  Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji. Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame. Aina za Choroko Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani. A) Choroko zinazotambaa , hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali. B) Choroko zinazosimama, hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusimama kwenda juu. Kipindi kizuri cha upandaji wa choroko Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga. Nafasi cha upandaji wa choroko na kiasi cha mbegu Choroko huit...