Posts

Showing posts from June, 2018

UFUGAJI BORA WA NG'OMBE WA MAZIWA

Image
Ndugu msomaji leo nitakuonyesha vitu vya muhimu vya kuzingatia pale unapo taka kuanza kufuga ng'ombe wa maziwa ,    UTANGULIZI ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ni moja kati ya ufugaji unao wakomboa wafugaji wengi sana endapo watazingatia kanuni za ufugaji bora mimi mwenyewe nimekua shahidi nikiona watu wengi wana piga hatua kutokana na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa  vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia sana wakati unataka kuanza na hata kama umeanza kufuga ng'ombe wa maziwa uchaguzi wa aina bora ya ng'ombe hili ni jambo la msingi sana kabla ya kuanza kufuga unatakiwa ujue je ni aina gani ya ng'ombe bora ambaye anaweza kunifaa . mwanzoni niliandika aina za ng,ombe wa maziwa hivyo sitopenda kurudia sana kuanza kuelezea aina za ng,ombe wa maziwa  nitaelezea kwa ufupi tu ukitaka kujua aina hizo kwa undani unaweza tafuta kwenye blog hii hii kwa kuandika  AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA. lakini kwa ufupi kuna aina tano kubwa ambazo zinatumika sana  fresian guersey jersey ...

Ufugaji Nyuki

Image
Ufugaji Nyuki Kwa kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula. Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki. Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengen...

KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

Image
Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo. Hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula. Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C. TABIA YA MMEA Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,. ENEO N...

UFUGAJI WA SAMAKI

Image
Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual) Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine. Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient) Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana. Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki k...

UFUGAJI BORA WA NGURUWE

Image
Habari mpenzi ,msomaji leo nataka nikuoneshe vitumuhimu katika ufugaji wa nguruwe kwa kua ni moja kati ya wanyama wenye faida sana. “Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa kisasa ili kupata nguruwe  bora.  Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo. Ufugaji Nguruwe hawa itaji mtaji mkubwa sana ili kuwafuga,hata wakulima wadogo  wanaweza kumudu kufuga nguruwe kwa kua huitaji mtaji mkubwa sana ili kuwa fuga na pia huleta faida kubwa pale wanapo fiki hatua ya kuya wakubwa BANDA Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa sakafu ya zege au ukachanganya mchanga na siment unaweza chagua kulingana na uwezo wako . Ukubwa wa banda unatege...

Jinsi Ya Kutengeneza Mbolea Ya Mboji Hatua Kwa Hatua

Image
Mboji ni nini? Mboji ni aina ya mbolea ya asili yenye rangi nyeusi na harufu nzuri ya kidongo ambayo hutokana na kuoza kwa mchanganyiko wa masalia ya mimea kunakosababishwa na vijidudu na wadudu rafiki wa mazao.  Muozo wa kutengeneza mbolea ya mboji ni tofauti na muozo wa kawaida kwa sababu muozo wa mboji unahitaji usimamizi ili kupata matokeo mazuri ambapo masalia ya mimea mbalimbali (ambayo kwa pamoja hutambulika kama malighafi) hukusanywa na kutengeneza biwi au lundo litakalooza na kuwa mboji kamili. Je ulishawahi kutumia mbolea ya mboji? Jibu laweza kuwa ndio. Lakini Je unajua jinsi ya kuandaa mbolea ya mboji? Kama ulikuwa unajiuliza swali hili basi umefika mahali sahihi. Hapa utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji. VITU VYA MSINGI KATIKA KUTENGENEZA MBOLEA YA MBOJI Vijidudu na Wadudu Sehemu kubwa ya lundo la mboji huozeshwa na vijidudu kama vile bakteria na fangasi ambavyo katika hali ya unyevu huitaji Kaboni (C) kama chanzo cha nishati na...

KILIMO CHA SOYA CHA KISASA

Image
1. UTANGULIZI Soya ni zao jamii ya mikunde ambayo ina baadhi ya sifa za mbegu zinazozalisha mafuta.   Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya juu kuliko iliyoko katika aina nyingine ya mazao ya mimea. Kiasi cha protini katika soya inazidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Sifa nyingine za zao la soya ni pamoja na kuwa na mafuta yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol), uwezo wa mmea wa soya kuongeza mbolea aina ya nitrojeni kwenye udongo, uwingi wa protini unaoweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha, uwezo wa soya kustawi katika maeneo yanayostawisha mahindi na maharage unamaanisha kwamba zao hilo linaweza kulimwa sehemu nyingi nchini Tanzania. Sifa hizo zimefanya zao la soya kuwa muhimu katika chakula cha binadamu na mifugo na katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za vyakula na madawa. Vilevile gharama za uzalishaji wa soya ni ndogo ukilinganisha na mazao mengine. Soya Pamoja na...