KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO
UTANGULIZI Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. viazi mviringo vina virutubisho vingi mfano vitamin, protin,madini na maji SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku mfano wa viazi mviringo AINA BORA YA VIAZI MVIRINGO Kuna aina nyingi sana ya viazi mviringo lakini hapa nitataja aina ambazo nazifahamu na ni bora kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole baraka sasamua tana subira(EAI 2329) Bulongwa kikondo(CIP 720050) ...