Posts

UFUGAJI BORA WA SUNGURA

Image
UTANGULIZI Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu MABANDA Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura. UFUGAJI WA NDANI 1 – Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha 2 – Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa...

UFUGAJI BORA WA SAMAKI

Image
UTANGULIZI  Ufugaji wa samaki unakua kwa kasi sana hapa nchini tanzania kutokana na kuonekana kua na faida sana. hivyo nimeamua leo nikupe elimu kidogo ambayo itakusaidia wewe mfugaji ambaye ungependa kujikita katika ufugaji huo, hivyo tue pamoja ili kujua mengi. SIFA ZA ENEO LA KUFUGIA SAMAKI Sio kila mahali hufaa kwa ufugaji wa samaki, ila mahali ambapo ni sahihi, zifuatazo ni sifa za eneo bora la kufugia samaki. eneo linalo fikika kwa urahisi eneo tulivu na lenye usalama wa kutosha eneo ambalo linavibali vyote vya umiliki lazima liwe na maji ya kutosha kwa kipindi chote utakacho fuga eneo ambalo halina mmomonyoko wala historia ya mafuriko eneo lenye uwezo wa kutuamisha maji eneo ambalo soko lake sio la shida UTENGENEZAJI WA BWAWA Kuna aina mbali mbali za kutengeneza mabwawa ya samaki inategemea na eneo, kiasi cha samaki unao taka kufuga, aina ya samaki na hali ya uchumi. aina hizo ni bwawa la kuchimba udongo bila kujengea(earthen pond)   bwawa la kuchimba...

Kilimo cha Nyanya Chungu

Image
 Zao hili pia hujulikana kwa jina la "Nyanya Chungu", "Ngogwe" au "Ntongo". Huu ni mmea wa kitropiki, na kustawi kwake karibu ni sawa na bilinganya. Mmea hukua na kufikia urefu wa meta moja hadi moja na unusu na matawi na majani yake hufanya kichaka. Nyanya mshumaa zinaweza kuwekwa katika makundi mawili: yaani aina itoayo matunda madogo madogo na machungu sana na aina itoayo matunda makubwa na machungu kidogo. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga zingine. Pia hupikwa pamoja na ndi. Kupanda: Miche huoteshwa kwa kupanda mbegu ambayo husiwa kwenye kitalu na kutunzwa kama mazao mengine. Miche ifikiapo kimo cha sentimeta 10 hadi 15 au majani manne 4 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50 kwa 75 au  sentimeta 9...

Jinsi ya Kuandaa Mbegu Ya Uyoga

Image
MAHITAJI: Unatakiwa kuwa na: Ø Chumba maalumu kisichopitisha mwanga Ø Presure cooker au jiko maalumu lenye moto mkali Ø Vyombo vya kuwekea mbegu kama vile glass Ø Maji salama Ø Ungaunga wa viazi vitamu Ø Uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu Ø Kibakuli kidogo chenye mfuniko na Ø Kipande cha uyoga (ambacho kitachanganywa na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu, kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga) HATUA YA KWANZA: Kuandaa fangasi 1. Changanya kipande cha uyoga na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu, kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga) 2.  Baada ya kuchanganya  mchangnyiko huo, chemsha mchanganyiko huo kwenye presha cooker au jiko la moto mkali. 3.  Ipua na weka mchanganyiko huo kwenye vibakuli vidogo vinne vyenye mfuniko 4.  Acha upoe kwa dakika kumi na tano. 5....

KILIMO CHA MIHOGO

Image
Zao la muhogo ni muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo na wenye kipato cha chini.Wakulima walio wengi huwa wanachanga zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde,mbaazi na njugumawe n.k. Muhogo hustawi zaidi katika maeneo yalipo kwenye mita 0 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari.Pia katika maeneo yanayopata mvua za wastani wa 750mm mpaka 1200mm.Muhogo ushamiri zaidi katika udogo wa kichanga na ustahimili hali ya ukame.Mikoa kama Lindi,Pwani,Tanga,Mwanza,Kigoma,Ruvuma,Morogoro,Mbeya na Shinyanga huwa kilimo cha mihogo kinakubali zaidi. MBEGU BORA YA MUHOGO Kutokana na wataalamu kuna aina mbili za mbegu ya muhogo ambazo zimethibitishwa na wakulima kama vile: (i)Naliendele; hizi ni mbegu ambazon mkulima akizitumia basi anakuwa na uhakika wa kupata tani 19 kwa hekta moja na inaweza kuvunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe. (ii)Kiroba; huzaa tani 25 mpaka 30 kwa hekta moja na pia inavunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe shambani. Mbegu hizi zin...

KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI

Image
Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu katika mlo wa familia za kitanzania, Afrika mashariki na Dunia nzima. Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari,kiungo cha mboga, nyama na samaki. Majani ya kitunguu pia hutumika kutengenezea supu n.k                                AINA ZA VITUNGUU MAJI Aina bora za vitunguu ni pamoja na Hybrid F1, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40kgs mpaka 60kgs kwa hekta.Mbegu bora katika zao la kitunguu ni Neptune F1, Jambar F1 pamoja na Rosset F1..Mbegu bora za vitunguu unawea kuzipata katika makampuni binafsi kama ya Kibo seed, Rotan seed, East Afrika seed company na kampuni za Balton na MASANTO katika kitengo cha mbegu. Pia unaweza kuzipata kwa wasambazaji wa mbegu pamoa na maduka ya TFA na maduka ya pembejeo za kilimo ka...

JIKWAMUE NA KILIMO CHA TANGAWIZI

Image
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro. Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k). . Aina za tangawizi Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi. Tabia ya mmea   Tangawizi ni mmea un...